Burudani

Wasichana wanajiuliza: Je, mshindi wa American Idol 2025 ameoa?

MISSISSIPI: USHINDI wa msimu wa 23 wa American Idol ulikwenda kwa Jamal Roberts, baada ya kuwashangaza majaji alipoimba wimbo wa Rick James ‘Mary Jane’.

Jamal Roberts ndiye mtu wa kwanza Mweusi kushinda ‘American Idol’ baada ya miaka 20 kupita. Lakini jambo la kushangaza ni kwamba wengi wakiwemo wanawake wamehoji kama Jamal ana mke ama la! Maana walionekana watoto wake watatu tu lakini mke wake hakuonekana walipokuwa wakifurahia ushindi wake.

Jamal akiandika, “Zaidi ya yote, natumai binti zangu wanaona hili na wanajua kwamba kwa imani, bidii, na moyo, chochote kinawezekana.”
Katika shindano hilo Jamal aliibuka mshindi wa kwanza na John Foster aliibuka mshindi wa pili.

“Mungu ni mwema sana. Tangu hatua yangu ya kwanza kwenye hatua hiyo hadi wakati huu wa kushangaza, sikuwahi kuota kwamba mtoto kutoka mji wangu siku moja angeitwa American Idol. Safari hii imekuwa kubwa kuliko mimi, na ninamshukuru sana kila mtu ambaye aliniamini nilipokuwa nikifuata ndoto hii.”

“Kwa jiji langu, familia yangu, na kila mtu huko nje. Ninapata kufanya muziki na walio bora zaidi ulimwenguni na kushiriki hadithi yangu. Lakini huu sio mwisho … ni mwanzo tu. Kutoka chini ya moyo wangu …. ASANTE!

Jamal anatoka katika mji mdogo unaoitwa Meridian, Mississippi. Jamal amefanya kazi kama mwalimu wa elimu ya viungo katika Shule ya Msingi ya Crestwood.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button