Burudani

Mke wa Ali Kiba achukizwa kauli ya Diamond

MKE wa msanii wa Bongo Fleva, Alikiba, Amina Khalef amelaani kitendo cha msanii Naseeb Abdul, ‘Diamond Platnum, kumkosea heshima kufuatia kumhusisha kwenye ugomvi wake na mumewe.

Diamond alitumia kauli iliyopokelewa tofauti wakati akimhusisha Amina kwenye majibu ya mfululizo ya mgogoro wake na Alikiba hali iliyozua sintofahamu na kumuibua Amina na kuandika;

“Ni jambo la kipuuzi, lenye nia mbaya, na la kustaajabisha kabisa kuhusisha watu wasio na hatia katika migogoro/visasi”.

“Ninalaani vikali ukosefu wa heshima kwa mwanamke. Bila hisia za heshima, hatuwezi kutofautisha wanaume na wanyama. Ni muhimu kuheshimu haki na hadhi ya kila mtu, bila kujali jinsia au asili yake.”

“Utu wema wa kibinadamu hauwezi kukiukwa”.

Related Articles

Back to top button