‘Wasanii waonywa kutumia vitu vya mitandaoni’

ZANZIBAR: WADAU wa sekta ya filamu nchini wamesisitizwa kukuza tasnia hiyo kwa weledi na umakini mkubwa pamoja na kuendelea kuimarika kwa masoko kupitia njia ya mtandao.
Kauli hiyo imetolewa katika Mdahalo muhimu ya uwezeshaji na biashara (monetization) uliofanyika kisiwani Unguja juzi katika Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) ambalo linaendelea kisiwani humo.
Mdahalo huo uliwaleta pamoja wadau muhimu kujadili changamoto na fursa katika tasnia ya filamu Tanzania katika dunia inayoshika kasi katika matumizi ya mtandao.
Mkurugenzi wa ZIFF, Khatib Madudu ambaye ndiye alikuwa muongozaji wa mdahalo amesema kwamba bila kuwa makini katika utawanyaji wa kazi katika mitandao kunaweza kuzuka mtafaruku katika Sanaa.
“Msipende kuchyukua kazi za watu wengine mnazoziona kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa zinaweza kuwaletea matatizo yatakayowakabili baada ya kutumia kazi za watu wengine kutoka mitandaoni hivyo wajitahidi kutengeneza kazi zao wenyewe.