Wasanii wabisha hodi Zanzibar kumuunga mkono Dk. Samia na Dkt Mwinyi

DAR ES SALAAM:WASANII wa Mama Ongea na Mwanao kwa kushirikiana na Lamata Village wameendelea kuonesha mshikamano wao wa kisiasa na kijamii baada ya kutangaza rasmi safari yao kuelekea Visiwani Zanzibar, wakimuunga mkono mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan na Dkt Mwinyi.
Awali, wasanii hao walitoa shukrani za dhati kwa wananchi wa mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa, Singida, Tabora na Kigoma kwa kujitokeza kwa wingi katika kampeni za Dk. Samia, jambo walilolieleza kuwa ni ishara ya imani kubwa ya Watanzania kwa uongozi wake.
Kwa mujibu wa wasanii hao, wameamua kujitoa kwa nguvu zote kuhakikisha Dk. Samia anaibuka kidedea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, ili aendeleze mazuri yaliyotekelezwa katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake.
“Tunataka kuhakikisha mama anaendelea na safari yake ya kuwatumikia Watanzania. Ameyafanya makubwa ndani ya muda mfupi, hivyo ni jukumu letu kumuunga mkono ili aendelee kutuletea maendeleo,” .
Baada ya kumaliza ziara ya bara, safari sasa inaelekezwa Zanzibar, ambako wasanii hao wanatarajia kushirikiana na wananchi katika shughuli za kampeni na kuhamasisha mshikamano wa kisiasa kwa ajili ya ushindi wa kishindo wa Dk. Samia.