Filamu

‘Wasanii achaneni na filamu za mapenzi,guseni changamoto za taifa’

ZANZIBAR: MWENYEKITI wa Bodi ya ZIFF, Chande Omari amewataka wasanii, wazalishaji na waongozaji wa filamu nchini kuachana na utengenezaji wa filamu za mapenzi kwa wingi badala yake watengeneze filamu zenye matukio yanayozigusa jamii nyingi kwa sasa nchini.

Mwenyekiti huyo amesema hayo katika uzinduzi wwa Tamasha la 27 la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF) linaloendelea visiwani hapa hadi Agosti 4.

Chande amesema wasanii wanatakiwa kujikita zaidi katika changamoto zinazosumbua taifa kwa sasa ikiwemo utekaji wa watoto, udhalilishaji wa watoto, ukosefu wa ajira, ugumu wa maisha kwa akina mama na mengine kama hayo na waachane na hadithi za mapenzi kwa filamu nyingi wanazofanya.

¨Tunakusudia kuwasukuma wasanii wa filamu waachane na filamu za mapenzi na badala yake waandae filamu zinazogusa jamii moja kwa moja ili zitatue changamoto zinazoendelea kulikumba taifa kwa sasa ikiwemo utekaji wa watoto, udhalilishaji, ukosefu wa ajira, ugumu wa maisha na mengine mengi,¨ amesema Chande.

Chande amesema ili kufanikisha hilo lazima serikali ishirikiane vyema na ZIFF kupitia wasanii watakaokuwa tayari kuandaa filamu hizo ili wapate maeneo wanayohitaji kwa ajili ya uandaaji wa filamu zao.

¨Bila kuwa na ushirikiano kutoka serikalini, hatutaweza kuandaa filamu hizo tunazotaka kuzifanya na kuondokana na filamu za mapenzi kwa sababu wasanii watataka maeneo ambayo umiliki ni wa serikali hivyo serikali inatakiwa ishirikiane nasi kwa kufungua milango yake ili tufanikishe uandaaji wa filamu hizo za changamoto kwa jamii,´´ alisema Chande.

Related Articles

Back to top button