Nyumbani

Wanufaika mikopo utamaduni na sanaa warejeshe-Chana

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dkt. Pindi Chana amewasisitiza wadau na wanufaika wa mikopo inayotolewa na Mfuko wa Utamaduni na Sanaa kurejesha mikopo hiyo kulingana na makubaliano.

Kwa mujibu wa wizara hiyo Chana ametoa agizo hilo leo alipofanya ziara Ofisi za mfuko huo.

“Nitoe rai kwenu wadau kutumia fedha hizo kwa ajili ya kazi zinazokusudiwa ili muendeleze kazi zenu,” amesema Chana.

Awali Afisa Mtendaji wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Nyakaho Mahemba amesema tayari mfuko huo umetumia takriban Shilingi bilioni moja kutoa mikopo kwa Wasanii.

Related Articles

Back to top button