Nyumbani

Wanasimba njooni mtusapoti

DAR ES SALAAM: KLABU ya Simba imeita mashabiki kuisapoti timu kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Petro Atletico ya Angola utakaochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam leo katika mkutano wa hamasa Msemaji wa Simba Ahmed Ally alisema mchezo huo una umuhimu kwao kuhakikisha wanashinda mbele ya umati wa mashabiki.

“Tuendelee kuhamasishana ili wanasimba wengi waje uwanjani Jumapili hii kutokana na umuhimu wa mchezo huu. Mpinzani wetu ni mkubwa kwelikweli na silaha yetu ni mashabiki, na tunajua nguvu yenu mkiujaza Uwanja wa Mkapa. Mkishakuja kwa wingi uwanjani tunamfanya vibaya Atlético de Luanda na hilo halina mjadala,”alisema.

“Kila Mwanasimba ni muhimu kununua tiketi na kuja uwanjani. Kama kuna mtu hajawahi kuja uwanjani basi huu ndio uwe mtoko wao wa kwanza. Jumapili Novemba 23 tuje uwanjani lakini tuhakikishe tumevaa jezi za msimu huu.”aliongeza.

Related Articles

Back to top button