EPL

Walker asaini miwili Burnley

LANCANSHIRE: Klabu ya Burnley iliyopanda daraja kushiriki ligi kuu ya England ametangaza kumsajili beki Kyle Walker kutoka Manchester City kwa mkataba wa miaka miwili.

Beki huyo wa kulia alikamilisha vipimo siku ya Ijumaa na atafanya kazi tena na kocha mkuu Scott Parker, ambaye walicheza pamoja Tottenham Hotspur kwa misimu miwili.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 alicheza mechi 15 katika nusu ya kwanza ya msimu uliopita akiwa na Man City kabla ya kujiunga na AC Milan kwa mkopo mwezi Januari, lakini klabu hiyo ya Italia iliamua kutofanya uhamisho wake kuwa wa kudumu.

Walker alishinda mataji 17 wakati akiwa Etihad na alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshinda Treble mwaka 2023. Alisajiliwa City msimu wa joto wa 2017 na alicheza mechi 319 Manchester city.

Burnley walipanda daraja kurejea Ligi kuu ya England msimu uliopita kufuatia kushuka daraja mwaka 2024.

Walker ni usajili wao wa tano msimu huu, baada ya kuwasili kwa beki Axel Tuanzebe, beki wa kushoto Quilindschy Hartman, kipa Max Weiss na winga wa Ufaransa Loum Tchaouna.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button