Nyumbani
Wadau wa michezo nendeni pembezoni kusaka vipaji

TANGA:MASHINDANO ya kandanda ya Samia Mkinga Cup 2025 yamefikia tamati huku wadau wakihizwa kwenda maeneo ya pembezoni kwa ajili ya kuibua vipaji vya soka badala ya kubaki mjini pekee.
Rai hiyo imetolewa na Mratibu wa mashindano hayo Said Omari (Duvii ) wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza Viwanja vya Mkinga Leo kushuhudia fainali hiyo.
Amesema maeneo ya pembezoni hususani wilaya ya Mkinga yanavipaji vingi ambavyo vinahitaji kuendelezwa ili vijana waweze kutimiza ndoto zao kupitia michezo.
“Tumefanya ligi hii ili vijana wapata ajira na kuonekana kwa sababu vipaji vingi vinaishia mashamba hivyo kupitia mashindano hayo Mkinga inakwenda kuandika historia ya kandanda kupitia vijana” amesema Duvii.