Africa
Wachezaji 24 Simba kwenda Uganda

KLABU ya Simba imewataja wachezaji 24 wanaoondoka leo jioni kwenda Uganda kuikabili Vipers katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika Februari 25.
Taarifa ya timu hiyo imewataka wachezaji hao kuwa ni magolikipa Aishi Manula, Beno Kakolanya na Ally Salum Juma.
Mabeki ni Shomari Kapombe, Israel Mwenda, Mohamed Hussein, Gadiel Michael, Kennedy Juma, Mohamed Outtara, Joash Onyango, Henock Inonga na Erasto Nyoni.
Viungo waliotajwa ni Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin, Clatous Chama, Ismael Sawadogo, Saidi Ntibazonkiza, Kibu Denis, Pape Osmane Sakho na Peter Banda.
Taarifa hiyo imewataja washambuliaji kuwa ni John Bocco, Jean Baleke, Moses Phiri na Habibu Kyombo.
Vipers itakuwa mwenyeji wa Simba kwenye uwanja wa St. Mary’s uliopo eneo la Kitende, Uganda.