Kwingineko
Vita fainali Ligi Mabingwa Ulaya

MAJIBU ya timu ipi itatwaa Kombe la Ligi ya Mabingwa ya Ulaya(UCL) yatapatikana leo wakati Borussia Dortmund itakapokabiliana na Real Madrid katika fainali kwenye uwanja wa Wembley, London, England.
Mchezo huo utachezeshwa na pilato Slavko Vincic kutoka Slovenia.
Kufika fainali Dortmund iliitoa Paris Saint Germain kwa jumla ya mabao 2-0 wakati Real Madrid iliiondoa Bayern Munich kwa jumla ya mabao 4-3.
Dortmund imetwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mara 1 pekee msimu wa 1996/97 ilipoifunga Juventus katika fainali.
Kwa upande wa Real Madrid, klabu hiyo ndio pekee iliyotwaa taji hilo mara nyingi zaidi ikifanya hivyo mara 14.