Mastaa

Usimchukie aliyekutangulia, jifunze kwake – Gabo Zigamba

DAR ES SALAAM:MSANII wa Bongo Movie, Gabo Zigamba, amewataka watu kuacha chuki kwa wale waliowatangulia katika maisha au taaluma zao, badala yake wawachukulie kama mfano wa kujifunza ili kufikia mafanikio makubwa zaidi.

Gabo ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram, ambapo amesema mtu aliyekutangulia hapaswi kuchukiwa, bali atumike kama darasa la kukuza maarifa na mipango bora ya mafanikio.

Kupitia ujumbe aliouchapisha, Gabo ameandika:
“Usimchukie mtu aliyekutangulia, mfanye mfano kama mchonga barabara, kisha jipange vyema kwa mafanikio zaidi yake. Na kama si lazima, basi usifeli hesabu ya mfano.”

Ujumbe huo umepokelewa kwa hisia chanya na mashabiki wake wengi, wakisema ni funzo muhimu la maisha, hasa kwa vijana wanaojitafuta katika nyanja mbalimbali za kazi na sanaa.

Related Articles

Back to top button