Michezo Mingine

UMSOTA yakabidhiwa sh milioni tano

DAR ES SALAAM: KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amekabidhi kiasi cha sh milioni 5 kwa timu ya Umoja wa Maveterani wa Soka Tanzania (UMSOTA) kama zawadi kutoka kwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan.

Amekabidhi fedha hizo Dar es Salaam jana katika hafla maalum ya kuipongeza timu hiyo baada ya kutwaa ubingwa wa mashindano ya soka ya Maveterani Afrika Mashariki, yaliyofanyika Oktoba 1, 2025 nchini Kenya.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UMSOTA Paul Lusozi maarufu kama ‘Father’ aliishukuru serikali kwa kutambua mafanikio yao, akiahidi kuwa timu hiyo itaendelea kushiriki mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuimarisha umoja na kukuza michezo miongoni mwa maveterani.

Mashindano hayo ya Afrika Mashariki yalihusisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini.

Related Articles

Back to top button