Ukivaaje unapendeza?
Nakshi ina nguvu kubwa mno kwenye mitindo, Nakshi zenyewe ninazozungumzia hapa ni kama miwani ya jua, cheni, hereni, saa, bangili na urembo mwingine.
Nakshi hizi unapozivaa kwa mpangilio mbali na kuongeza unadhifu hukufanya upendeze zaidi.
Hata kama umevaa nguo ambazo sio nadhifu sana unapoongezea vitu kama hivyo hukufanya kuonekana maridadi.
Unachotakiwa kufanya ni kujua jinsi ya kupangilia kuanzia chini hadi juu.
Ninapozungumzia kupangilia ni pamoja na kujua jinsi ya kuchagua vitu hivyo kulingana na nguo unazotaka kuvalia na eneo unalokwenda.
Kwa mfano si kila nguo ya kuvalia hereni kubwa, au bangili au saa fulani.
Au si kila mtu anaweza kuvaa miwani ya fasheni fulani hii itategemea na aina ya nguo uliyovaa lakini pia ile inayoendana na umbile na uso wako.
Kama unakwenda ofisini au kanisani, msikitini hakikisha unavaa hereni ndogo, na saa simple.
Unapohitaji kwenda kwenye mitoko ya usiku au sherehe unayo nafasi nafasi ya kuvaa hereni kubwa na bracelet zinazong’aa.
Kwa upande wa miwani ivaliwe wakati wa jua tu kama miwani yenyewe ni ya jua