
TIMU ya taifa ya soka (Taifa Stars) leo imevuna alama muhimu baada ya kuilaza Uganda Cranes goli 1-0 katika mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON) uliopigwa Ismailia, Misri.
Goli hilo limefungwa na Simon Msuva katika dakika ya 68. Mchezo wa marudiano utafanyika Tanzania Machi 28.
Kwa matokeo hayo sasa Tanzania inashika nafasi ya pili katika kundi F ikiwa na alama 4 huku Algeria ikiongoza kwa alama 9, Niger ikiwa ya 3 kwa alama 2 na Uganda ni mwisho ikikusanya alama 1.