Africa
Twiga Stars yainyoa Ivory Coast
TIMU ya taifa ya soka kwa wanawake (Twiga Stars) imesonga mbele katika michuano ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake(WAFCON 2024) baada ya leo kutoa Ivory Coast kwa mikwaju ya penalti 4-2.
Hatua hiyo ya penalti imefikiwa baada ya Twiga Stars kushinda kwa mabao 2-0 katika mchezo wa marudiano kwenye uwanja wa Azam Compelx, Dar es Salaam hivyo kuwa sawa kwa mabao 2-2 kufuatia ushindi wa Ivory Coast wa mabao 2-0 Septemba 22.
Kwa matokeo hayo Twiga Stars sasa inasubiri hatua inayofuata kupambana na timu kati ya Togo na Djibouti.