World Cup
Ufaransa vs Morocco nani kumfuata Argentina fainali?
NUSU fainali ya pili ya michuano ya Kombe la Dunia Qatar 2022 inapigwa leo kwenye uwanja wa Al Bayt uliopo jiji la Doha.
Mchezo huo utaamua timu gani itapambana na Argentina iliyotangulia fainali baada ya kuichapa Croatia kwa mabao 3-0 Desemba 13.
Mechi hiyo itaamuliwa na César Arturo Ramos Palazuelos wa Mexico akisimama katikati huku akisaidiwa na mwamuzi namba moja Alberto Morín Méndez wakati namba mbili atakuwa Miguel Ángel Hernández Paredes.
Iwapo Morocco itafanikiwa kutinga fainali, hiyo itakuwa rekodi mpya kwa timu kutoka Afrika kufuzu nusu na kisha fainali ya Kombe la Dunia tangu michuano hiyo kuanzishwa mwaka 1930.




