World Cup

Tuungane na kuiombea Serengeti Girls-Balozi Mbega

Balozi wa Tanzania nchini India, Anisa Mbega.

BALOZI wa Tanzania nchini India, Anisa Mbega ameisifu timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 17(Serengeti Gilrs) licha ya kupoteza mechi dhidi ya mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia, Japan.

Katika mchezo wake kwanza wa mashindano hayo yanayofanyika India, wawakilishi hao wa Tanzania walikubali kipigo kizito cha 4-0 huko Goa Kusini Magharibi mwa Mji Mkuu, New Delhi.

“Sisi tuliokuwa pale uwanjani tulishuhudia, hawa vijana wamejitahidi sana, lakini nimezungumza na Kocha, amenihakikishia watajipanga ili waweze kufanya vizuri zaidi,” HabariLeo Online imemnukuu Balozi.

Hata hivyo, amemmiminia sifa kipa wa Serengeti Girls kwa ushupavu aliouonesha kwa kuzuia michomo kutoka kwa washambuliaji wa Japan.

Akielezea Japan, Mwanadiplomasia huyo amesema timu hiyo ina wachezaji waliojengeka hivyo kitendo cha kuruhusu magoli hayo tu Tanzania imejitahidi kwani India iliwahi kuchabangwa 8-0.

Ametoa wito kwa Watanzania kuungana na kuiombea timu hiyo ili iweze kufanya vema katika mechi zilizobaki.

Tanzania ipo kundi D ambapo mchezo unaofuta utakuwa Oktoba 15 dhidi ya Ufaransa na kisha Canada Oktoba 18.

Related Articles

Back to top button