BurudaniMuziki

Tshala Muana afariki dunia

MWANAMUZIKI mashuhuri wa Jamhuri ya Kidemorasi ya Congo Élizabeth Tshala Muana Muidikay, maarufu Tshala Muana amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kinshasa.

Mzalishaji wa muziki ambaye pia ni mume wa msanii huyo aliyekuwa na umri wa miaka 64, Claude Mashala alikuwa wa kwanza kutoa taarifa ya kifo cha Tshala Muana.

“Leo asubuhi, Mungu amechukua maisha ya Tshala Muana. Roho yake ipumzike kwa amani,” amesema Mashala kupitia ukurasa rasmi wa Facebook.

Ndugu wa Tshala Muana, Jean-Marie Kassamba amethibitisha kifo cha mwanamuzki huyo.

Ripoti zimesema Muana ambaye alikuwa amelazwa hosptali kwa wiki moja amefariki dunia kutokana na matatizo ya kupumua.

Muana ambaye pia alijulikana kwa jina la ‘Mamu Nationale’ katika Jamhuri ya Kidemorasi ya Congo likiwa na maana ya ‘Mama wa Taifa’ aliwahi kupata tuzo kadhaa kupitia nyinmbo zake zikiwemo Karibu Yangu, Malu, Tshianza, Dezo Dezo na Tshibola.

Related Articles

Back to top button