EPLKwingineko
Tottenham yamwinda Kompany

Habari zimesema Kocha wa Burnley Vincent Kompany amekuwa kipaumbele cha kwanza cha Tottenham Hotspur kuchukua nafasi ya Antonio Conte aliyetimuliwa ukocha mwezi uliopita.
Nahodha huyo wa zamani wa Manchester City amesimamia mabadiliko makubwa katika klabu ya Burnley msimu huu baada ya klabu hiyo kushushwa daraja msimu uliopita.
Burnley imepanda daraja kucheza Ligi Kuu England msimu ujao baada ya kukusanya pointi 90 ikiwa imebakiza michezo saba Ligi ya Championship kumalizika.
Imedaiwa kuwa Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy, binafsi amefurahishwa na jinsi Kompany alivyoiongoza Burnley kurejea EPL ikicheza mtindo makini na wa kuvutia.