
KOCHA Mkuu wa Simba, Juma Mgunda amesema tofauti ya pointi iliyopo kati ya timu hiyo na Yanga katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara inachangia wachezaji wake kucheza kwa presha.
Akizungumza na SpotiLeo, kocha huyo amesema wachezaji wa wa Simba wanahofia kupoteza mchezo jambo ambalo ameahidi kulifanyia kazi kwenye mechi zijazo.
“Kitendo cha Yanga kutuacha pointi sita kinawasumbua wachezaji wangu kiasi cha kutocheza kwa uhuru uliozoeleka wakihofia kupata matokeo tofauti na pointi tatu,” amesema Mgunda.
Amesema yeye kama kocha mkuu atajitahidi kuwajenga kisaikolojia wachezaji wake ili waweze kukaa sawa na kucheza kwa kufuata maelekezo anayowapa.
Simba ipo nafasi ya tatu katika msimamo wa ikiwa na pointi 31 na michezo 14 wakati watani wao Yanga wamekusanya pointi 32 huku wakicheza mechi 12 na wana mechi mbili mkononi ambazo ni sawa na pointi sita iwapo watashinda.