Tiwa Savage: Ujauzito uliathiri sauti ya albamu yangu

LAGOS: MWIMBAJI maarufu wa Nigeria, Tiwa Savage, amesimulia jinsi ujauzito ulivyoathiri sauti yake.
Alifahamisha haya alipokuwa akizungumzia uzoefu wake wa ujauzito kama mwanamuziki kwenye Afrobeats Intelligence.
Savage alieleza kuwa mapambano yake na safu ya sauti yalimfanya abadilishe baadhi ya note za kuimbia katika albamu yake ya ‘R.E.D’.
“Nilikuwa mjamzito niliporekodi ‘R.E.D’ nilikuwa studio nikilia na tumbo langu kubwa.Ilikuwa tabu kurekodi albamu.
“Nilibadilisha sauti za baadhi ya nyimbo kwenye albamu kwa sababu kuwa mjamzito kuliathiri jinsi nilivyoweza kupiga noti.
“Nilikuwa mtu wa kwanza kupata mtoto huko Mavin, kwa hivyo kila walipoona nguvu zangu zinapungua, Jazzy ambaye ni boss wa Mavin aliwaambia wasaidizi wake wanipatie mayai na mkate kasha niliendelea hadi albamu ikakakamilika”, alisimulia.
DAILY POST inaripoti kwamba mwimbaji huyo alijiunga na lebo ya Don Jazzy, Mavin Records mnamo 2012 na akaondoka kujiunga na Universal Music Group mnamo 2019.