Muziki

Tiwa Savage: Sitamwacha mwanaume kwa usaliti

LAGOS: MKALI wa muziki wa Afro Beat kutoka Nigeria, Tiwa Savage, amezua gumzo baada ya kufunguka kuwa hawezi kuachana na mwanaume wake kwa sababu ya usaliti wa kimapenzi, isipokuwa iwapo mwanaume huyo atahusishwa na vitendo vya uhalifu kama wizi au matumizi ya dawa za kulevya.

Akimzungumzia msimamo wake kupitia moja ya podcast, Tiwa Savage amesema kuwa katika maisha yake hajawahi kumsaliti mwanaume, wala kuvunja uhusiano kwa sababu ya kusalitiwa na mwanamke mwingine.

Amesema kuwa mara nyingi mwanaume kuwa na mwanamke mwingine “si kwamba hakupendi, bali huwa ni tamaa,” na kwamba kitendo hicho hakimfanyi athibitishe kupungua kwa mapenzi katika uhusiano.

Hata hivyo ameweka wazi kuwa hatoweza kuvumilia uhusiano na mwanaume anayejihusisha na makosa makubwa kama wizi, biashara au matumizi ya dawa za kulevya, akisisitiza kuwa hilo ni jambo linalovuka mipaka ya maadili na usalama.

Kauli hiyo imeibua mjadala mtandaoni kuhusu mipaka ya uvumilivu katika mahusiano, huku wengi wakitoa maoni tofauti kuhusu mtazamo wa msanii huyo.

Related Articles

Back to top button