Ligi Daraja La Kwanza

Timu ya gofu JWTZ kushiriki mashindano ya dunia Marekani

Wachezaji tisa wa Klabu ya Gofu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Lugalo wanatarajia kuliwakilisha jeshi hilo katika Mashindano ya Dunia ya Majeshi Santiego nchini Marekani Oktoba mwaka huu.

Akizungumza Mwenyekiti wa Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo amewataja wachezaji hao kuwa ni Kapteni Chediel Msechu, Kapteni Samuel Mosha, Marius Kajuna, Samuel Kileo, John Hiza, Nsajigwa Mwansasu na Kwa Wanawake ni Letisia Kapalila, Zumla Hamisi na Hadija Selemani.

Brigedia Jenerali Mstaafu Luwongo amesema Wachezaji waliopata nafasi watashiriki Mashindano ya Mufindi Open, Morogoro Open na kuweka Kambi Jijini Arusha Mwezi wa Tisa lengo ikiwa kurejea na ushindi.

Kwa upande wake Meja Japhet Masai(Nahodha wa Klabu) amesema kuwa Miongoni mwa Wachezaji waliopata nafasi wamesema,changamoto zilikuwa kubwa viwanjani lakini kupitia mazoezi na kujituma imewawezesha kufanya vizuri.

Naye John Hiza amesema Mchakato wa Kuwatafuta wachezaji watakaoliwakilisha Jeshi na Nchi katika Mashindano hayo ya Dunia ya Majeshi Mwezi Oktoba Nchini Marekani limehitimishwa tayari Kwa ajili ya Kambi

Related Articles

Back to top button