Tetesi

Tetesi za usajili

WEST Ham huenda ikajitoa kwenye majadiliano ya kumsajili Harry Maguire kutoka Manchester United kutokana na dili hilo kuchukua muda mrefu kukamilika. Wiki iliyopita klabu hizo mbili zilikubaliana vipengele vya ada ya pauni milioni 30 lakini maendeleo ya kumaliza uhamisho yamekuwa polepole.(Guardian)

Licha ya kukubaliana dili la pauni milioni 60 na Southampton, Liverpool inatarajiwa kukosa kumsajili Romeo Lavia anayekwenda Chelsea. The Reds pia imeshindwa kumsajili kiungo wa Brighton Moises Caicedo aliyesaini The Blues.(The Athletic)

Hivi karibuni Chelsea imejitoa kwenye dili kumsajili Tyler Adams kutoka Leeds, huku Liverpool pia ikihusishwa naye lakini yupo katika mpango wa kujiunga na Bournemouth kutokana na The Cherries kutarajiwa kuhuisha kipengele cha kumwachia cha pauni milioni 20.(BBC Sport)

Vilabu vinavyoshiriki Ligi ya kulipwa Saudi Arabia vina nia kumsajili beki wa Arsenal, Gabriel Magalhaes. Iwapo Mbrazil huyo ataondoka, The Gunners inaweza kuamua kumfukuzia Aymeric Laporte wa Manchester City au Marc Guehi wa Crystal Palace.(Daily Mirror)

Bayern Munich, Chelsea, Manchester City, Manchester United na Real Madrid zimekosa nafasi kumsajili Neymar JR kutoka PSG, huku Mbrazil huyo akikamilisha usajili klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia.(Independent)

Tottenham Hotspur inatarajiwa kutuma ombi la kwanza kwa ajili ya kumsajili nyota wa Gent Gift Orban ambaye anaonekana kuwa mbadala wa muda mrefu wa Harry Kane. Hata hivyo Spurs inataka kuuza baadhi ya wachezaji kabla ya kipaumbele cha kusajili wapya.(Evening Standard)

Mshambuliaji mwingine aliyeko kwenye rada ya Tottenham ni Folarin Balogun ambaye anatarajiwa kuruhusiwa kuondoka kutoka wapinzani Arsenal majira hayo ya joto kwa ada ya pauni milioni 50.(Gazzetta dello Sport)

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button