Teknolojia yatajwa msisimko CWC

NEW YORK, Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya FIFA Pierluigi Collina amesifu utendaji Kamera za mwili kwa waamuzi, sheria mpya ya sekunde nane kwa walinda mlango, na teknolojia ya hali ya juu ya offside ya Semi-Automated Offside Technology zinazotumika kwenye Kombe la Dunia la Klabu
Michuano hiyo ambayo inafanyika kwa upanuzi wa hadi timu 32 kwa mara ya kwanza imekuwa tukio la kwanza la ki Soka FIFA kutumia kamera za mwili kwa waamuzi huku Collina akisema uvumbuzi huo umevuka matarajio ya kamati yake ukitoa muonekano wa kipekee kwa watazamaji wa televisheni na kusaidia mafunzo ya waamuzi.
“Matokeo ya kutumia kamera ya mwamuzi kwa marejeo hapa kwenye Kombe la Dunia la Klabu yamevuka matarajio yetu. Tulifikiri lingekuwa jambi la kuvutia kwa watazamaji wa TV na ni kweli tumepokea maoni mazuri. Lakini sasa inatusaidia kuwafunza waamuzi pia kwa sababu tunaona kile mwamuzi anakiona” – Amesema
Michuano hiyo pia ilishuhudia utekelezaji wa sheria ya kutoa mpira wa kona ikiwa golikipa hataanzisha mchezo na kushikilia mpira kwa zaidi ya sekunde nane. Hapo awali, ‘free kick’ pekee ililotolewa baada ya Golikipa kuzuia mpira kwa sekunde sita Collina akisema imeongeza msisimko kwenye mechi.
Kuboreshwa kwa teknolojia ya Semi-Automated Offside Technology kumerahisisha maamuzi ya sheria hiyo tata zaidi kwenye Soka huku ikizuia uchezaji usio na lazima na kupunguza matumizi ya VAR kwenye matukio hayo.
Jumla ya wasimamizi wa mechi 117 – waamuzi 35, waamuzi wasaidizi 58 na maafisa wasaidizi wa video (VAR officials) 24 kutoka vyama 41 wanachama wa FIFA wamesimamia mechi 63 zilizochezwa wakati wa mashindano hayo.