Kwingineko
‘Asante José’
KLABU ya Roma ya Italia imetangaza kuvunja mkataba na Kocha wake Mkuu José Mourinho.
Taarifa ya Roma imesema Mourinho ataondoka klabu hiyo pamoja na timu yake nzima ya ufundi.
“Kwa niaba ya kila mmoja katika klabu ya AS Roma, asante José!,” imesema taarifa hiyo.
Katika michezo kumi ya mwisho Ligi Kuu Italia, Roma imeshinda mitano, sare miwili na kufungwa mara tatu ikiwa na pointi 29, ikishika nafasi ya tisa baada ya michezo 20.