Michezo MingineNyavuRiadha

Tanzania yaanza na mguu mzuri Olimpiki Maalumu

TIMU ya Tanzania ya Olimpiki ya mpira wa wavu kwa wanawake imeanza vyema kampeni yake katika michuano ya Olimpiki maalumu kwa kuibuka na ushindi wa alama 25-10 dhidi ya Italia katika mchezo wa awali wa kufuzu hatua ya pili ya mchujo kwenye michuano hiyo inayoendelea nchini Ujerumani.

Michuano hiyo maalumu inafanyika katika mji wa Berlin nchini Ujerumani ambapo mataifa mbalimbali yanashiriki , Waziri wa  utamaduni sanaa na Michezo Dkt Pindi Chana alikuwa shuhuda wakati bendera ya Tanzania ikipepea nchini Ujerumani.

Mwanariadha Mathias Makanyaga kutoka Tanzania ameshika nafasi ya tatu kwenye mbio za mita 800 na hivyo kufuzu fainali ambapo kesho atatupa karata yake fainali akikimbia mita 800.

Katika mchezo mwingine timu ya wanaume ya mpira wa wavu imepoteza alama 17-16 dhidi ya timu ya Botswana lakini timu hiyo imesonga mbele katika hatua inayofuata.

Related Articles

Back to top button