
TIMU ya taifa ya wanaume chini ya miaka 23 leo inaikabili Nigeria katika mchezo wa marudiano kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON) mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Liberty uliopo Ibadan, Nigeria.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.
Tanzania inahitaji ushindi wa bao 1-0 au sare ya zaidi ya mabao 2-2 kwenye mchezo huo utakaofanyika saa 12 jioni ili kufuzu.
Mechi nyingine za michuano hiyo leo ni kama ifuatavyo:
Zambia vs Sierra Leone
Gabon vs Magadascar
Algeria vs DR Congo
Ivory Coast vs Niger
Mali vs Rwanda
Senegal vs Burkina Faso