Nyumbani

Tabora United yatangaza vita nafasi nne ligi kuu

TIMU ya soka ya Tabora United imesema licha ya kuanza vibaya kwa kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa Azam FC na sare na Singida Fountain Gate bado ina nafasi ya kugombea nafasi nne za juu katika Ligi Kuu.

Msemaji wa Klabu hiyo, Pendo Lema amesema kwa kuwa hawataki kushuka daraja hivyo lazima wapambanie nafasi nne za juu ili wajiweke vizuri katika ligi hiyo yenye ushindani mkubwa.

“Hatufikirii kushuka daraja tunawachezaji 12 wakigeni, 16 wandani jumla tuna wachezaji 28 watakaotuvusha kufikia lengo yetu la nafasi za juu,” alisema lema.

Pendo aliongeza kwamba wapo kiushindani ndiyo maana wamesajiri wachezaji waliowaniwa na timu kongwe nchini kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Eswatini, Nigeria na Congo.

“Takriban miaka 10 sasa tangu Rhino Rangers iliposhuka daraja wakazi wa tabora hawakuwa na timu ya Ligi Kuu, Tabora United hatutaki kuwatia unyonge wana Tabora tutapigania nafasi nne za juu na hatushuka daraja” alisema Pendo.

Related Articles

Back to top button