Spurs kumsajili Porro kwa bil 123/-

KLABU ya Tottenham Hotspur imekubali dili la kumsajili nyota wa Sporting Lisbon, Pedro Porro kwa pauni milioni 42 sawa na shilingi bilioni 123.6 huku mchezaji huyo akitarajiwa kwenda London leo kufanyiwa vipimo.
Dili hilo lilionekana kuwa katika shaka baada ya Sporting kufuta uhamisho huo licha ya mpango wa vipimo kufanyika.
Porro anayecheza nafasi za beki wa kulia au winga wa kulia alikacha mazoezi huku akishinikiza uhamisho huo.
“Naishukuru Sporting, naipenda klabu, sikufanya mazoezi kwani nililenga tu uhamisho kwenda Spurs lakini nitaendelea kuishukuru klabu,” Porro ameviambia vyombo vya habari vya Ureno.
Porro amefunga mabao matatu na kusaidia 11 katika mashindano yote msimu huu na ameimarisha nafasi yake kama mmoja wa wachezaji muhimu wa Sporting.