Europa

Spurs kumkosa Son tena

LONDON, Meneja wa Tottenham Hotspur Ange Postecoglou amesema nahodha wa kikosi hicho Son Heung-min atakosa mechi ya mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Europa League dhidi ya Bodo/Glimt utakaopigwa katika Uwanja wa Tottenham Hotspur kesho Alhamisi

Son hajacheza Spurs tangu kikosi chake kilipopata sare ya 1-1 mbele ya Eintracht Frankfurt Aprili 10 mwaka huu kutokana na jeraha la mguu licha ya kocha wake kuelezea matumaini ya kuwa naye wiki iliyopita na kwamba mshambuliaji huyo wa mwenyeji wa Korea Kusini angeweza kurejea kwa ajili ya mchezo huu.

“Son hatacheza kesho usiku, Yuko mazoezini lakini bado hajaanza mazoezi ya pamoja na timu. Anaimarika na tunatumai tutamrejesha mapema zaidi.” alisema Postecoglou alipozungumza na wanahabari kuelekea mchezo huo.

Son amefunga mabao 11 katika mechi 43 msimu huu, lakini hakuna bao linalotokana na ‘open play’ kutoka kwake tangu tarehe 23 Januari. Spurs walipokea kichapo cha 19 kwenye Ligi wakifedheheshwa katika Uwanja wa Anfield Jumapili baada ya kubomoka 5-1 wakiwa daraja la Liverpool wakitawazwa mabingwa.

Kipigo hicho kilichotabiriwa kiliwafanya wabaki nafasi ya 16 kwenye msimamo wa Ligi wakiwa kwenye eneo baya zaidi kumaliza ligi tangu waliposhuka kwenye Ligi Kuu ya Englandmwaka 1977, ingawa hawawezi kushuka daraja mara hii.

Related Articles

Back to top button