
BAADA ya michezo mitatu nyumbani Singida Big Stars leo itakuwa mgeni wa Geita Gold kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara.
Singida Big Stars inashika nafasi ya 5 ikiwa na pointi 7 baada ya michezo 3.
Geita Gold ipo nafasi ya 14 ikiwa na pointi 2 baada ya michezo 3 pia.
Septemba 20 kumefanyika mchezo mmoja wa ligi hiyo ambapo KMC ikiutumia uwanja wake wa nyumbani wa Uhuru, Dar es Salaam imeifunga Ihefu kwa mabao 2-1.