Africa

Simba yakemea mapepo, haitaki mazoea

DAR ES SALAAM: MFALME wa nyikani, Simba tayari ameondoka nchini kuifuata Al Masry ya Misri kwenye robo fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika itakayopigwa Aprili 02, 2025.

Wakati kikosi cha Simba kinaondoka kimeacha ujumbe mzito kwa mashabiki wa timu hiyo.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema wanakwenda Misri kutengeneza njia ya kwenda nusu fainali kwani wanaamini ikiwa watapata matokeo mazuri ugenini kazi itakuwa nyepesi nyumbani.

Kocha wa Simba Fadlu David’s amesema shauku ni kutwaa taji hilo lakini kwasasa wanakwenda hatua kwa hatua na kituo kinachofuata ni Al Masry.

Simba ina kisiki kigumu mbele kilichodumu kwa zaidi ya miaka saba ambapo wanakwama katika hatua ya robo fainali lakini imani yao inawaambia kuwa mzimu uliowatesa tangu mwaka 2018 sasa unakwenda kufika tamati.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button