Ligi Ya WanawakeNyumbani
Simba Queens, Yanga Princess viwanja tofauti SLWPL leo
LIGI Kuu ya wanawake Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo mitano kupigwa viwanja tofauti.
Simba Queens ipo ugenini jijini Dodoma kuikabili Fountain Gate Princess kwenye uwanja wa Jamhuri huku Alliance Girls ikiikaribisha Yanga Princess kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
The Tigers Queens itakuwa mwenyeji wa Baobab Queens kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wakati Mkwawa Queens ni wageni wa Amani Queens kwenye uwanja wa Ilulu mkoani Lindi.
Nayo JKT Queens itakuwa nyumbani uwanja wa Maj Gen Isamuhyo mkoani Dar es Salaam kuikabili Ceasiaa Queens.




