Ligi Ya WanawakeNyumbani
Simba Queens, Yanga Princess viwanja tofauti leo

LIGI kuu ya soka kwa wanawake inaendelea leo kwa michezo mitano kupigwa viwanja tofauti.
Simba Queens ipo ugenini mkoani Mwanza kukipiga dhidi Alliance Girls kwenye uwanja wa Nyamagana.
Nayo Yanga Princess ni mgeni wa JKT Queens inayoongoza ligi hiyo kwenye uwanja wa Maj Gen Isamuhyo,Dar es Salaam.
The Tigers Queens itakuwa mwenyeji wa Amani Queens kwenye uwanja wa Black Rhino uliopo Karatu mkoani Arusha.
Wakati Baobab Queens ya mkoani Dodoma itakuwa ikivaana na Mkwawa Queens kwenye uwanja wa Chuo cha Mkwawa, Iringa, Fountain Gate Princess itakuwa mwenyeji wa Ceasiaa Queens kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.