EPL

Scholes asimulia ugomvi wake na Ferguson

LONDON, ENGLAND: KIUNGO wa zamani wa Manchester United, Paul Scholes amefichua kuwa aliamini maisha yake ya soka yangefikia mwisho baada ya ugomvi wake na kocha wa zamani wa timu hiyo Sir Alex Ferguson mwaka 2001.

Scholes amefichua hayo wakati wa mahojiano maalum kwenye podcast ya mchezaji mwenzie wa zamani wa Manchester United Nicky Butt inayofahamika kama Football’s Greatest Eras.

Paul amesema alijipata pabaya baada kufanya kosa lililomkasirisha meneja huyo anayeheshimika zaidi kwenye ulimwengu wa soka.

Scholes amesema alitokea benchi katika mchezo dhidi ya Newcastle united wakiwa nyuma kwa mabao 3-1 kisha wakapunguza moja lakini zikiwa zimesalia dakika 20 pekee kosa lake lilimfanya mchezaji wa Newcastle united Alan Shearer kutanua uongozi kuwa mabao 4-2 katika mchezo huo wa msimu wa 2001/02.

“Aliniita na kunitukana sana, aliniita majina ya ajabu. Sijui nilipatwa na nini nikajikuta kwenye majibizano nae, unajua nina heshima sana mimi si mtu wa kujibizana na mtu kama Fergie lakini bila sababu yoyote nilijikuta namjibu”

“Aliniambia hutakaa ucheze tena kwenye hii timu, nikamwambia sijali. Baada ya mechi nilikaa kwenye basi usiku ule nikajisemea nimekwisha nadhani Jumatatu asubuhi nitasaini kwingine” amesema Scholes.

Scholes aliyehitimisha safari yake ya soka mwaka 2013 alikuwa sehemu muhimu ndani ya kikosi cha Sir Alex Ferguson akiisaidia Manchester united kushinda mataji 11 ya Premier League matatu ya kombe la FA na mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Related Articles

Back to top button