Filamu

Salman Khan aahirisha ziara ya Manchester baada ya shambulio India

MUMBAI: MUIGIZAJI wa India Salman Khan ameahirisha ziara yake ya Bollywood Big One nchini Uingereza kutokana na shambulizi la kigaidi la Pahalgam lililotokea nchini India.

Ziara hiyo ilipangwa kufanyika Mei 4 na 5 huko Manchester na London. Muigizaji huyo wa Sikandar alituma ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram akishiriki bango la ziara hiyo yenye neno ‘imeahirishwa’.

Ziara hii inajumuisha waigizaji Madhuri Dixit Nene, Varun Dhawan, Tiger Shroff na Kriti Sanon. Sara Ali Khan, Disha Patani, Maniesh Paul na Sunil Grover pia watashiriki pamoja na Salman Khan katika ziara hiyo.

Ziara ya Bollywood Big One ilipangwa kufanyika Mei 4 kwenye Ukumbi wa Co-op Live huko Manchester, ikifuatiwa na onyesho mnamo Mei 5 kwenye OVO Arena ya London.

Muigizaji huyo amesema kwamba amefanya uamuziki mgumu kuahirisha ziara hiyo kutokana na shambulio la Pahalgam wiki iliyopita. Ameomba radhi mashabiki wake kwa usumbufu uliojitokeza kwao na amesema tarehe mpya za ziara hiyo zitatangazwa hivi karibuni.

“Kwa kuzingatia matukio ya hivi majuzi ya kusikitisha huko Kashmir, na kwa huzuni kubwa, tumechukua uamuzi mgumu wa kuahirisha maonesho ya ‘The Bollywood Big One’, ambayo yalipangwa kufanyika Mei 4 na 5 huko Manchester na London,” Salman Khan aliandika.

“Ingawa tunaelewa ni kwa kiasi gani mashabiki wetu walikuwa wakitazamia maonesho haya, tunaona ni vyema kusitisha wakati huu wa malalamishi. Tunaomba radhi kwa kutamaushwa au usumbufu wowote ambao unaweza kusababisha na tunathamini sana uelewa na usaidizi wako. Tarehe mpya za maonyesho zitatangazwa hivi karibuni,” aliongeza.

Related Articles

Back to top button