Rosey Manfere: Mimi Bado mdogo, bado sifikirii ndoa

DAR ES SALAAM: MISS Tanzania 2020, Rosey Manfere, amesema bado ni mdogo kiumri na anajivunia kuwa sehemu ya kizazi cha Generation Z, akieleza kuwa vijana wa kizazi hicho wamekuwa wachangamfu na kufanya vizuri katika nyanja mbalimbali ikilinganishwa na kizazi cha Millennial.
Rosey amesema kwa sasa hana shinikizo la kuingia kwenye ndoa, akisisitiza kuwa kauli zake zilizotafsiriwa vibaya hazikumaanisha kuwa yupo single, bali alieleza tu kuwa bado hajafikia hatua ya ndoa.
Amefafanua kuwa mwaka huu ametimiza umri wa miaka 26, hivyo bado anajiona kijana na mwenye muda wa kujijenga zaidi katika maisha yake binafsi na taaluma.
“Mimi sikusema niko single, nilisema ndoa hamna. Mimi ni Gen Z, hata miaka 27 sijafika.Nimetimiza miaka 26 mwaka huu,” amesema Rosey.
Miss Tanzania huyo amesema vijana wa Generation Z wana ari, ubunifu na uwezo mkubwa wa kuendana na mabadiliko ya dunia ya sasa, hali inayowafanya kung’ara katika maeneo mengi ya kijamii na kiuchumi. Ameongeza kuwa kwa sasa anajikita zaidi katika kujijenga, kutimiza malengo yake na kutumia fursa zinazojitokeza, huku akiamini kuwa kila jambo lina wakati wake sahihi.




