EPLEuropaKwinginekoLa LigaSerie A

Ronaldo ndio basi tena Ulaya

NAHODHA wa timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo amefuta uwezekano wa kurejea tena kusakata soka barani Ulaya  na kusema ligi ya Saudi Arabia  ni bora kuliko ligi ya Marekani ambayo nyota Lionel Messi amejiunga nayo.

Kwa mujibu wa mtandao wa ESPN  kauli hiyo  imekuja mara baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Celtavigo  ambapo timu yake ilibugizwa bao 5-0.

“Nina uhakika wa 100%  siwezi  kurudi kwenye klabu yoyote barani Ulaya nina miaka 38 kwa sasa, Mpira wa Ulaya umepoteza ladha yake ligi ambayo inafanya vizuri na ina ubora kwa sasa ni ligi kuu ya England pekee” amenukuliwa Ronaldo

Ronaldo ameongeza kuwa Ligi ya Saudi Arabia ni bora kuliko ligi ya Marekani  na ndio sababu wachezaji  wengi wakubwa wanatimkia huko  na anamini ndani ya mwaka mmoja ligi hiyo itapasua anga zaidi na kuzipita baadhi ya ligi za Ulaya.

Mshindi huyo wa tuzo ya mchezaji bora ulimwenguni Ballon dior mara tano alijiunga na Al Nassr  Desemba 2022 baada ya kuachana na Manchester United na baada ya uhamisho wake nyota  wengi wanatua kwenye ligi hiyo.

Related Articles

Back to top button