World Cup
		
	
	
Robo fainali ya kibabe Kombe la Dunia
						MICHEZO miwili ya awali ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia inapigwa leo jijini Doha, Qatar.
Mabingwa mara tano Brazil itakaibili Croatia kwenye uwanja wa Education City huku miamba ya soka Argentina ikivaana na Uholanzi kwenye wa uwanja wa Lusail.
Timu zitakazoshinda michezo hiyo zitakutana katika nusu fainali.
Hadi kuingia hatua hiyo Brazil imeitoa Korea Kusini hatua ya 16 bora kwa mabao 4-1 wakati Argentina ikiitoa Australia kwa mabao 2-1.
Nayo Uholanzi imeitoa Marekani kwa mabao 3-1 wakati Croatia imetoa Japan kwa penalti 3-1.
				
					



