Kwingineko

Rashford roho safi na United

BARCELONA, mshambuliaji mpya wa FC Barcelona Marcus Rashford aliyetua klabuni hapo kwa mkopo kutoka  Manchester United amesema hana kinyongo wala maneno mabaya kwa klabu yake hiyo iliyomlea.

Akizungumza kwenye hafla ya utambulisho wake uliofanyika katika Uwanja wao wa Spotify Camp Nou jijini Barcelona Rashford amesema United inapitia kipindi cha mpito ikiutafuta ukali wake ambao klabu hiyo imepoteza kwa muda mrefu.

“Manchester United inapitia kipindi cha mpito, wamekuwa katika hali hiyo kwa muda sasa. Lakini United imekuwa sehemu kubwa si tu ya kazi yangu, bali maisha yangu pia… Sina jambo baya la kusema kuhusu Manchester, na ninashukuru kwa nafasi niliyopewa ya kuichezea.”
Nawatakia mafanikio katika siku zijazo.”

Rashford amekuwa na ingia-toka nyingi kwenye kikosi cha Mancheter United kabla ya kutua Barça Rashford alitumia nusu ya pili ya msimu uliopita kwenye mkopo mwingine na Aston Villa

Raia huyo wa England atakuwa na mabingwa hao wa Laliga kwa msimu mzima huku mkataba huo wa mkopo ukiwa na kipengele cha kumnunua moja kwa moja chenye thamani ya Euro milioni 30.

Related Articles

Back to top button