Rais uefa awatolea uvivu Saudi Arabia.

RAIS wa shirikisho la soka barani Ulaya Aleksander Ceferin ametema nyongo kwa taifa la Saudi Arabia kwa kitendo chao cha kuendelea kuwasajili wachezaji wenye majina makubwa kutoka Ulaya.
Cerefin amesema usajili wanaofanya Saudi Arabia ni makosa makubwa kwenye soka lao kwani walipaswa kuwekeza kwenye soka la vijana kuliko kutumia fedha nyingi kuwasajili wachezaji ambao wanakaribia kumaliza soka lao.
“kununua wachezaji wanaomalizia soka lao sio mfumo wa kuendeleza soka, kosa kama hilo walilifanya China”,amesema Cerefin.
Timu mbalimbali kutoka Saudi Arabia zimetenga fungu la maana kwa ajili ya kufanya usajili ambapo tayari nyota kadhaa wamenasa kwenye mtego wa pesa kutoka Uarabuni akiwemo Cristiano Ronaldo aliyenaswa na Al-Nassr pamoja na Karim Benzema aliyejiunga na Al- Ittihad.