Kwingineko
PSG nyumbani, Bayern ugenini UCL leo

MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa Ulaya(UCL) hatua ya 16 ya inaendelea leo kwa michezo miwili.
Miamba ya Ufaransa, Paris Saint-Germain itakuwa uwanja wa nyumbani, Parc des Princes, uliopo jiji la Paris kuikaribisha Real Sociedad ya Hispania.
Bayern Munich ya Ujerumani itakuwa mgeni wa Lazio ya Italia kwenye uwanja wa Olimpico jijini Rome.
Katika michezo miwili ya kwanza hatua ya 16 bora Februari 13, Manchester City ikiwa ugenini imeichapa FC Copenhagen mabao 3-1 wakati Real Madrid pia ikiwa ugenini imeshinda bao 1-0 dhidi ya RB Leipzig.