Ligi KuuNyumbani

Prisons yaitupa gerezani Polisi

MAAFANDE wa Tanzania Prisons leo wameutumia vyema uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya kujinyakulia pointi 3 baada ya kuichapa Polisi Tanzania mabao 2-0 katika mfululizo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania bara.

Mabao ya Prisons katika mchezo huo yamefungwa na Jeremiah Juma mkwaju wa penalti dakika 5 huku la pili likifungwa na mshambuliaji Samson Mbangula dakika ya 45 baada ya kupokea pasi ya Juma.

Matokeo hayo yameipandisha Prisons hadi nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi wakifikisha pointi 12 katika michezo nane.

Kipigo cha leo kimeirudisha mkiani mwa msimamo wa ligi Polisi Tanzania ambayo tangu kuanza kwa msimu huu imeshinda mchezo mmoja pekee kati ya mechi tisa iliyocheza wakikusanya pointi 5.

Related Articles

Back to top button