
LIGI Kuu ya soka Tanzania Bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja jijini Mbeya.
Tanzania Prisons inaikaribisha Coastal Union katika uwanja wa Sokoine jijini humo.
Prisons inashika nafasi ya 8 ikiwa na pointi 14 baada ya michezo 10 wakati Coastal ipo nafasi 13 ikiwa na pointi 8 baada ya michezo 7.
Novemba 9 kulifanyika michezo miwili ya ligi hiyo ambapo Simba imetoka sare ya bao 1-1 na Singida Big Stars katika uwanja wa LITI mjini Singida huku Azam ikishinda mabao 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji katika uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.