
KOCHA Mkuu wa Polisi Tanzania, Mwinyi Zahera amesema sare ya mabao 3-3 iliyopata katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting imeipa timu hiyo matumaini ya kushinda mchezo dhidi ya Namungo Januari 2, 2023.
Akizungumza na SpotiLeo, Zahera amesema marumaini hayo yanatokana na wachezaji wake kuanza kushika vyema mbinu na maelekezo anayowapa kwenye uwanja wa mazoezi.
“Tunacheza na Ruvu ni timu nzuri lakini Polisi hii siyo ile tuliyocheza na Yanga au na Simba, timu imeimarika kwa kiasi kikubwa naamini tutawashangaza watu kwa matokeo tutakayoyapata kwenye mchezo huo,” amesema Zahera.
Amesema pamoja na timu yake kuwa mkiani mwa msimamo wa ligi lakini haiwezi kushuka daraja kutokana na maingizo mapya ambayo wamekusudia kuyaleta kwenye usajili wa dirisha dogo.
Polisi Tanzania imeshinda michezo miwili pekee, kupoteza michezo 12 na sare michezo minne ikiiwa na pointi 10.