Nyumbani

Pamba Jiji yajichimbia Morogoro

MOROGORO: KLABU ya Pamba Jiji imeanza maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu kwa kuweka kambi maalumu mkoani Morogoro, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha kikosi chake kabla ya kuanza kwa mashindano rasmi.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao ya kijamii, Pamba Jiji imethibitisha uwepo wake Morogoro kwa maandalizi hayo ya msimu mpya hatua inayolenga kuimarisha kiwango cha wachezaji kimwili na kiufundi sambamba na kuongeza mshikamano wa kikosi.

Kocha Mkuu wa timu hiyo Francis Baraza anatarajiwa kutumia kambi hiyo kwa mazoezi ya nguvu, majaribio ya mbinu mpya na mechi za kirafiki ambazo zitawapa wachezaji nafasi ya kupata muunganiko mzuri kabla ya kuanza kwa ligi.

Kambi hiyo pia inatarajiwa kutoa fursa kwa benchi la ufundi kuchambua wachezaji wapya waliojiunga na kikosi hicho, pamoja na kuimarisha nidhamu na morali ya timu kuelekea msimu unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Pamba imeachana na wachezaji wengi iliokuwa nao msimu uliopita baadhi yao wakiwemo Ibrahim Isihaka, Modou Camara, Lazaro Mlingwa, George Mpole, Cherif Ibrahim, Abalkassim Suleiman, Paul Kamtewe, Mwaita Gereza, Deus Kaseke na Ally Ramadhan.

Imesajili wachezaji wapya kama Siwa Oyugi, Arijifu Amour, Hassan Kibailo, John Wawu, Abdallah Hamis, Amos Kadikilo, Abdallah Idd na Abdulmajid Mangalo.

Related Articles

Back to top button