Serie A

Palladino, Fiorentina wapeana ‘talaka’

FLORENCE: MABINGWA wa zamani wa Serie A Fiorentina wametangaza kuwa aliyekuwa kocha wao Raffaele Palladino ameihama klabu hiyo ya Serie A kwa makubaliano ya pande zote mbili baada ya kuifundisha klabu hiyo kwa msimu mmoja pekee.

Iliripotiwa mapema wiki hii kwamba Palladino aliwasilisha barua ya kujiuzulu kwake kwenye ngazi za juu za klabu hiyo lakini klabu ilianza jitihada za kumbakisha klabuni hapo kocha huyo mwenye umri wa miaka 41 ambaye amewawezesha kumaliza wa 6 msimu huu na kucheza Conference league msimu ujao.

Taarifa fupi iliyotolewa na klabu hiyo imethibitisha kwamba mkataba wa Raffaele Palladino, pamoja na ule wa benchi lake la ufundi, umesitishwa kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Kuondoka kwa Palladino ni pigo kwani aliiwezesha Fiorentina kumaliza katika nafasi ya sita kwenye Serie A, nafasi ambayo inawawezesha kushiriki Conference League msimu ujao. Huku msimu huu ukitajwa kuwa msimu wa mafanikio. Fiorentina pia ilifika nusu fainali ya Conference League ikiwa imepoteza katika fainali ya michuano hiyo katika kila misimu miwili iliyopita, chini ya kocha wa sasa wa Bologna Vincenzo Italiano.

Related Articles

Back to top button