Ligi KuuNyumbani

Ongala nje Azam, wawili wang’oka Simba

MOTO wa wachezaji na benchi la ufundi katika klabu za Ligi Kuu Tanzania kuondoka unazidi kuwaka ambapo leo Azam na Simba zimeachana na makocha watatu.

Kocha Msaidizi wa Azam Kali Ongala amepewa mkono wa kwaheri katika klabu hiyo ya Chamazi, Dar es Salaam.

“Thank you for your memories! 🙏Ahsante sana kwa utumishi wako uliotukuka ndani ya klabu yetu kocha wetu, @kali_ongala.Kazi yako itakumbukwa daima kwenye historia ya klabu yetu! Tunakushukuru sana na tunakutakia kila la kheri katika maisha yako mapya ya soka”, imesema.

Tayari Azam imeachana na Kocha wa magolikipa Dani Cadena na wa viungo Dk Moadh Hiraoui huku ikiwapa mkono wa kwaheri wachezaji watano ambao ni Bruce Kangwa, Kenneth Muguna, Rodgers Kola, Cleophace Mkandala na Islamil Aziz.

Kwa upande wa Simba, timu hiyo imeachana makocha wa viungo na wa magolikipa.

“Asante kwa Kelvin Mandla ambaye alikuwa kocha wetu wa viungo. Tunakushukuru kwa muda wote uliokuwa nasi. Asante kocha wetu wa magolikipa, Chlouha Zakaria kwa muda wote uliokuwa sehemu ya benchi letu la ufundi. Tunakutakia kila la kheri katika maisha yako mapya nje ya Simba,” imesema ya Simba.

Juni 14 Yanga imetangaza Kocha wake Mkuu Nasreddine Nabi kuondoka klabu hiyo baada ya kuomba kutoongeza mkataba mpya.

Related Articles

Back to top button